Habari
Freeman Mbowe aonekana kwa mara ya kwanza Dodoma

Mwenyekiti Mstaafu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Freeman Mbowe akiwasili katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma, kushuhudia uzinduzi wa Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050.
Katika hafla hiyo inayofanyika leo Julai 17, 2025 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan atakuwa mgeni Rasmi katika tukio hilo la kihistoria linalotokea kila baada ya miaka 25.





