Habari

Galaxy Z Flip5 na Galaxy Z Fold5 rafiki wa mazingira

Samsung Electronics Co. Ltd inaendelea kujivunia uwepo wa kizazi chake cha tano cha simu za Galaxy zinazofunguka (foldables): Galaxy Z Flip5 na Galaxy Z Fold5 katika soko la Tanzania ambazo zimezingatia na kutoa kipaumbele kwa suala la utunzaji wa mazingira.

Utengenezaji wa simu hizi imara na zilizotokea kupendwa na watumiaji wengi, umezingatia na kufanyika kwa aina maalu. ya plastiki ambayo ni imara na iliyochakatwa kwa asilimia 80 ambayo ina muonekano kama glasi inayopendezesha upande wa nyuma wa simu hizi.

Lakini pia simu hizi zina glasi zuri ambalo linapendeza na uchakataji wake umefanyika kwa asilimia 22.

Kitufe cha kupandishia na kupunguza sauti kimetengenzwa kwa plastiki maalumu ambayo uchakataji wake umefanyika kwa asilimia 20. Vyote hivi vinazifanya simu hizi ziwe rafiki kwa watumiaji lakini pia kwa mazingira.

#GalaxyZFlip5 #GalaxyZFold5 #JoinTheFlipSide @samsungtanzaniaO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents