Uncategorized

Gambo afanikisha Maulid ya Wilaya Arusha


Mbunge wa Arusha Mjini, Mrisho Gambo ameshiriki sadaka ya kufanikisha Maulid inayotarajiwa kufanyika kesho Novemba 27 katika msikiti wa Riyadh, Kata ya Muriet Wilaya ya Arusha.

Akitoa sadaka hiyo leo Nov 26, Mh. Gambo amesema kwamba amefurahi kushiriki katika kufanikisha shughuli hiyo, ambayo itaendana na shughuli za kijamii.

Amesema licha ya kufanyika kwa Maulid hapo Muriet lakini pia zitafanyika shughuli za uchagiaji damu pamoja na vipimo vya afya kwa watu wote jambo ambalo linagusa jamii yote kwa ujumla.

Katika kuhakikisha Maulid hiyo inafanikiwa Mh. Gambo amechangia Kanzu 200 kwa ajili wa viongozi hao wa dini wa wilaya, ng’ombe wawili, mchele kilo 800, maji nk.

Pamoja na hayo Mbunge huyo amesisitiza ataendeleza ushirikiano na viongozi wa dini zote pale atakapohitajika, na kusisitiza baada ya shughuli ya Maulid amejianda kupeleka msaada wa Krismass katika vituo vya watoto yatima na wenye uhitaji.

Kwa upande wa Viongozi wa Bakwata wamemshukuru kiongozi huyo ambapo wamesema kutokana na mahitaji yao Mbunge huyo ameweza kuchangia kwa asilimia 95 na kuomba aendelee kujitoa pale wanapokuwa na uhitaji.

BY : Fatuma Muna

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents