Michezo

Gamondi aonyesha Jeuri – Edo Kumwembe

Mechi ya Kaizer Chiefs Gamondi alitupa ujeuri wa namna mbili. Kwanza kilikuwa ni kikosi ambacho kiliendelea kubadilika kutokana na mahitaji uwanjani. Ile ndoto ya mashabiki kuwaona Clatous Chama, Pacome Zouzoua, Maxi Nzengeli na Azizi Ki wakicheza kwa pamoja imezidi kutokomea. Gamondi anatumia akili yake na sio ya mashabiki.

Lakini hapohapo Gamondi ameendelea kuwa jeuri kwa namna ambavyo anataka wachezaji wake watimize majukumu wasipokuwa na mpira. Huu umeendelea kuwa ubora wa Yanga kwa muda mrefu. Kuanzia wakati wa Nabi hadi wakati huu wa Gamondi. Bahati nzuri kwa Yanga ni kwamba Gamondi anaonekana kuwa master zaidi. Kaizer wangeweza kucheza siku MBILI wasione nyavu za Djigui Diarra

Na sasa tumeshaiona Yanga kwa mechi tatu. Wanarudi na taji lao la Toyota baada ya kuwasha moto pale Bloemfontein. Inatia hamu kusubiri kuona watani wao wamejiandaaje. Kuanzia uwezo wa mchezaji mmoja mmoja kwa wale ambao ndio kwanza wameingia kikosini hadi uwezo binafsi wa kocha na mipango yake.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents