Michezo

Gamondi humwambii kitu kwa Guede

Kocha wa Klabu ya Yanga Miguel Gamondi mara baada ya ushindi dhidi ya Polisi Tanzania wa mabao 5-0, alionesha kufurahishwa kwake na namna mshambuliaji wake mpya Joseph Guede kwa kuingia kambani mara mbili katika ushindi huo.

Gamondi amesema “Sikumpa presha, niliongea na Guede nikamwambia unapaswa kufunga, nakusapoti, unajua wakati mwingine unakosa nafasi nikamwambia tulia mabao yatakuja tu.”

“Kiukweli Guede ni straika mzuri, anafiti kabisa katika mfumo wetu wa uchezaji. Ni mzuri katika mipira ya juu kimbinu ni mzuri pia, kwetu yeye (Guede) na Okrah usajili wao katika dirisha dogo ni mzuri sana.” Kocha Miguel Gamondi.

Mchezo unaofuata wa Yanga Sc ni katika michuano ya Klabu Bingwa Afrika wakiwa nyumbani kwenye Uwanja wa Benjamini Mkapa watamkaribisha CR Belouizdad ya Algeria siku ya Jumamosi tarehe 24/2/2024 majira ya saa 1:00 Usiku.

Mpaka sasa Wananchi wakiwa katika kundi D wamefanikiwa kukusanya alama 5 tu baada ya kucheza michezo 3 wakiwa wanashika nafasi ya tatu katika kundi hilo wakiongozwa na kinara AL Ahly ya nchini Misri wakiwa na alama 6, akifuatiwa na CR Belouizdad akiwa na alama 5 sambamba na Yanga Sc huku Medeame kutoka Ghana wakiwa mkiani mwa kundi hilo na alama zao 4.

Mpaka sasa kwenye michuano ya Klabu Bingwa Afrika kila timu imebakiza mechi mbili ili kumaliza hatua hizo za makundi, timu pekee iliyofuzu kwenda Robo fainali mpaka hivi sasa ni moja tu nayo ni Asec Mimosas ya nchini Ivory Coast wakiwa vinara wa kundi B na alama zao 10 wakifuatiwa na Simba kutoka Tanzania mwenye alama 5 na Jwaneng Galaxy mwenye alama 4 akiwa watatu kwenye kundi hilo huku kigogo Wydad Casablanca akiwa na alama 3 tu.

Simba siku ya Ijumaa tarehe 23/2/2024 atakuwa dimbani ugenini kiminyana na Asec Mimosas katika Uwanja wa Stade Felix Houphouet-Boigny majira ya saa 4:00 Usiku.

Asec Mimosas wanatarajia kumkosa nyota wao Sankara Karamoko aliyetimkia Ulaya huku Simba wakitarajiwa kuwakosa nyota wake watatu Willy Onana, John Bocco wakiwa na majeraha pamoja na Ayoub Lakred ambaye anatumikia adhabu na atakosa mchezo mmoja tu.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents