Habari
Gari la shule latumbukia Mtoni

Mwanafunzi mmoja amefariki dunia huku wengine saba wakiwa hawajulikani walipo na Watu wengine watatu kupelekwa Hospitali baada ya gari ya shule ya Ghati Memorial kutumbukia mtoni majira ya asubuhi katika Kata ya Sinoni Mkoani Arusha.
Mkuu wa Wilaya ya Arusha Felician Mtahengerwa amesema wanamshikilia Dereva wa gari hiyo huku chanzo cha ajali hiyo ikidaiwa kuwa ni Dereva huyo kulazimisha kupita kwenye daraja hilo baada ya Wananchi kumzuia kupita kutokana na mafuriko.
Imeandikwa na Mbanga B.