Habari

Getrude Mongela ataka Samia akosolewe kibinadamu

Aliyekuwa Rais wa kwanza wa Bunge la Umoja wa Afrika, Balozi Getrude Mongella amesema akitokea mtu mwenye ujasiri wa kumkosoa Rais Samia Suluhu, basi amkosoe kutokana na mapungufu ya kibinaadamu na siyo kwakua ni mwanamke.

Balozi Mongella ameyasema hayo leo wakati akizungumza kwenye Kongamano la Kumbukizi ya Hayati  Mwl. Julius Nyerere linayofanyika huko mkoani Geita, Wilaya ya Chato.

Amesema anajisikia vibaya sana kuzungumzia umuhimu wa mwanamke kwenye jamii kila wakati kwa kuzingatia pia Rais anayeongoza nchi kwa sasa ni Mwanmke shupavu na mwenye maono makubwa kwa nchi yake.

Balozi Mongella amesisitiza kwamba endapo Rais Samia akipewa ushirikiano wa kutosha ataonyesha vipaji vikubwa vya wanawake katika kutenda kazi.

Pamoja na hayo Balozi Mongella amewakumbusha anawake kwamba wakati ndio huu wa kuchapa kazi “wakina mama sasa ndio kumekucha kabisana kina baba nyie tulieni kuleni raha”.

BY : Fatuma Muna

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents