Gigy Money akiwa na baibui baada ya kutoka Polisi, Masha Love amfariji (Video)
Msanii wa muziki Gigy Money baada ya kusekeseke lake na baba mtoto wake na baadae kwenda Polisi, jioni ya leo amenaswa na kamera za mapaparazi akitoka Osterbay Polisi kwa siri.
Gigy ambaye alivalia baibui jeusi alitoa shingo nje katika gari ambalo lilimbeba na kuelekea nyuma ya jengo là Msasani Mall.
Baada ya muda mfupi Gigy alinaswa akisalimiana na rafiki yake Masha Love na kutokomea kusikojulikana.
Mwanasheria wa msanii huyo wakati anatoka katika kituo cha polisi cha Ostabay alifuatwa na mwandishi wetu lakini alikataa kuzungumza chochote.
Bongo5 ilimtafuta Kamanda wa Polisi Kinondoni RPC Mtatiro ambaye alisema yupo kwenye kikao.
Bado tunaendelea kufuatilia tukio ili kujua kinachoendelea.
Mapema leo Mo J alitoa tamko kwamba anakwenda kumshitaki muimbaji huyo kwa madai kutokana na matusi aliyotukanwa kupitia mitandao ya kijamii.