Michezo

Girumugisha kumng’oa Adebayor Singida

SINGIDA Black Stars inapiga hesabu kali za kumbeba winga wa Al Hilal, Jean Claude Girumugisha ili atue katika kikosi hicho kuchukua nafasi ya Victor Adebayor waliye mbioni kumsitishia mkataba alionao mwishoni mwa msimu huu.


.
Adebayor aliyeanza kuitumikia timu hiyo mara dirisha dogo la usajili lilipofunguliwa Disemba mwaka jana, ameshindwa kuonyesha makeke wala kupenya katika kikosi cha kwanza, jambo linalowafanya mabosi wa klabu hiyo kufikiria kumsitishia mkataba wa miaka? miwili alionao kwa sasa.


.
Mabosi wa Singida wanatafuta mbadala wake mapema ili kuona kama wanaweza kupata saini ya Mrundi huyo, mwenye mkataba wa miaka mitatu ya kuitumikia Al Hilal. Taarifa za ndani zinaeleza kuwa; “Jina la winga huyo liko mezani likijadiliwa ili kuona jinsi gani tutamng’oa kwa Waarabu hao na kuwa naye msimu ujao.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents