HabariMichezo

Golden State Warriors mabingwa NBA

Usiku wa jana bingwa wa ligi ya NBA amepatikana ambapo timu ya mpira wa kikapu ya Marekani Golden State Warriors imetwaa ubingwa wa NBA 2022 kufuatia ushindi wa vikapu 103 kwa 90 dhidi ya Boston Celtics katika mchezo wa sita wa fainali hizo na kufanya matokeo ya michezo 6 Warriors kushinda michezo 4 na Celtics kushinda michezo 2 kati ya michezo saba.

Huu ni ubingwa wa saba kwa Warriors wakichukua ubingwa miaka ya 1975, 2015, 2016, 2017, 2018, 2019 na 2022.

Lakini kubwa zaidi ni kwamba ni Ubingwa wa 4 katika miaka 8 kitu ambacho ni mafanikio makubwa sana kwa timu hiyo inayotoka San Fransisco.#Bongo5Updates

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents