Michezo

Good News Yanga na Aziz Ki

Taarifa itakayowashusha presha mashabiki wa Yanga ni kwamba hatimaye kiungo mshambuliaji wa timu hiyo Stephanie Aziz Ki amewasili nchini huku akitolewa Uwanja wa Ndege kininja zaidi.

Aziz Ki amewasili nchini Alfajiri ya leo Julai 10, 2024 akitokea mapumzikoni kwao Burkina Faso kwa Ndege ya Shirika la Ndege la Ethiopia lakini akatoka kimkatati Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere terminal 3.

Alichofanya Aziz Ki, kwanza akamtanguliza ,fanyakazi ,,oja wa Uwanja wa Ndege mbele na mabegi yake makubwa sita aliyotua nayo.

Hatua ya pili ikiwa Ofisa mmoja wa Yanga Godlisten Anderson (Chicharito) aliyekuja kumpokea uwanjani hapo kumpenyezea kofia maarufu kwa jina la kepu, ambayo kiungo huyo ilimfikia akatoka akiwa ameishusha kijanja mithili ya mtu asiyetaka kujulikana.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents