
Kocha wa Manchester City, Pep Guardiola amewapa hongera majirani zake Manchester United kwa kutwaa taji la Carabao Cup.
Imepita miaka sita bila Man United kushinda taji huku Guardiola akiwa na Man City wakishinda makombe tisa yakiwemo ya Premier League na League Cup.
”Hongera kwa United kushinda Carabao Cup pamoja na Newcastle, wameonyesha mchezo mzuri.”- Guardiola ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari.