Michezo
Guede atia Mkwara
Mshambuliaji mpya wa Singida Black Stars, Joseph Guede aliyekuwa akikipiga Yanga msimu uliopita amechimba mkwara mpema akisema anatarajia msimu bora kutokana na wachezaji waliopo. . “Nafurahia maisha ndani ya Singida. Nimekutana na vipaji vingi vikubwa na naamini nitakuwa na msimu mzuri kutokana na kuizoea ligi na kuwa kwenye kikosi cha wachezaji wengi wenye uchu wa mafanikio,” .
“Kuhusu kuizungumzia Yanga na usajili walioufanya sio rahisi kwani sasa ni wapinzani wangu. Napenda kuzungumzia timu niliyopo ambayo nina furaha nayo na natarajia mambo makubwa nikiwa na timu hii ambayo imeniamini.”
. Akizungumzia bao la kwanza alilofunga akiwa na timu hiyo kwenye tamasha la Singida Big Day dhidi ya Aigle Noir, alisema “Mimi ni mshambuliaji kazi yangu ni kufunga na hakuna mchezaji ambaye anacheza nafasi kama yangu anaingia uwanjani kwa lengo la kuchezea mpira tu bila kufunga nimejiunga na Black Stars kwa lengo la kuhakikisha naipambania inafikia malengo,” alisema mchezaji huyo.