Burudani

Gwiji wa muziki wa Reggae, rafiki wa Bob Marley afariki dunia 

Mwanamuziki huyo, kutoka Kingston, Jamaica, alikuwa mmoja waanzilishi wa bendi ya The Wailers pamoja na rafiki yake wa utotoni, Bob Marley.

Bunny Wailer

Bunny Wailer alishinda tuzo tatu za Grammys
Kwa pamoja, walipata umaarufu kimataifa kupitia nyimbo zao za reggae kama vile Simmer Down na Stir It Up, kabla ya Wailer kujiondoa mwaka 1974.

Aliendelea mbele na kushinda tuza tatu za Grammys na kutunukiwa Tuzo ya heshima ya Jamaica 2017.

Kifo chake kilithibitishwa na maneja wake Maxine Stowe, na Waziri wa Utamaduni wa Jamaica, Olivia Grange.

Chanzo cha kifo chake hakijulikani, lakini alikuwa amelazwa hospitali tangu alipougua kiharusi Julai 2020.

Mashabiki wake wamekuwa wakimuomboleza nguli huyo wa muziki wa Reggae, baadhi yao wakimtaja kama shujaa.

“Mungu ambariki Bunny Wailer,”aliandika Red Hot Chill Peppers bassit, Flea wrote Red Hot Chili Peppers bassist, Flea. ” Mwamba wa kweli na mtu mzuri. Nampenda sana.”

Waziri Mkuu wa Jamaica Andrew Holness, Pia alimuombolea, na kutaja kifo chake kuwa “pigo kubwa kwa Jamaica na ulimwengu reggae”.The Wailers

Kikundi cha awali cha The Wailers, circa 1964 Kushoto -kuelekea kulia-R): Bunny Wailer, Bob Marley and Peter Tosh

Nyota huyo, ambaye jina lake halisi ni Neville O’Riley Livingston, alikuwa mwanachama wa mwisho wa bendi ya The Wailers aliyekuwa hai, baada ya kifo cha Bob Marley mwaka 1981 katokana na saratani, na kuuawa kwa Peter Tosh katika kisa cha wizi wa mabavu mwaka 1987.

Livingston alikulia kijiji cha Nine Miles, ambako alilelewa na baba yake aliyekuwa akiuza mboga.

Ni katika kijiji hicho alipokutana mara ya kwanza na Marley, na wawili hao wakatokea kuwa marafiki wakubwa utotoni, ambapo walitunga muziki wao wa kwanza wakiwa shule ya msingi ya Stepney na shule ya upili.

Kufuatia kifo cha baba yake Marley mwaka 1955, mama yake, Cedella, aliolewa na baba yake Livingston.

Awali wavulana hao walilelewa kama ndugu wa kambo hasa baada ya Cedella na Thaddeus kumzaa binti yao, Pearl.

Walipohamia Trenchtown Kingston, walikutana na Peter Tosh na kubuni kundi la uimbaji la The Wailing Wailers – kwa sababu, Marley alisema: “Tulianza kwa kulia.”

Eneo hilo lilikuwa masikini na lilikumbwa na ghasia. Livingston baadae anakumbuka kutengeza gita lake la kwanza kutokana na “fimbo ya mianzi, waya laini kutoka kwa kebo ya umeme na mtungi mkubwa”.

Lakini Muibaji Joe Higgs, maarufu “the Godfather of Reggae”, ambaye alikuwa akiishi karibu aliwachukuwa vijana hao na kukuza vipaji vyao.

Chini ya uelekezi wake, waliboresha sauti yao, wakaungana na waimbaji wengine kama vile Junior Braithwaite, Beverly Kelso na Cherry Green kabla ya kufupisha jana lao kuwa The Wailers.

Mwezi wa Decemba 1963, bendi hiyo iliingia studios ya Coxsone Dodd maarufu Studio One kurekodi wimbo wa Simmer Down, ambao uliandikwa na Marley kutoa wito wa amani katika makazi duni ya Kingston.

The Wailers baadae walitambulika kupitia wimbo huo ambao ulipata umaarufu sana nchini Jamaica. Walifua na toleo asili la Duppy Conqueror, kabla ya kutoa albamu yao ya kwanza The Wailing Wailers, mnamo 1965.

Lakini walifanikiwa kutoa nyimbo 28 kati ya mwaka 1966 na 1970, kabla ya kuachia albamu yao ya pili inayofahamika kama, Soul Rebels.

Mafanikio yao ya kimataifa yalikuja miaka mitatu baadaye na kibao chao cha Catch A Fire – rekodi ya kwanza waliyoifanya na Chris Blackwell katika chini ya lebo ya Island Record.

Ushirikiano uliotokana na changamoto zilizokumba bendi yao wakati huo. The Wailers walizuru Uingereza katika tamasha la muziki na Johnny Nash – ambaye baada ya wimbo wao wa Stir It Up kuvuma – lakini walashindwa kulipia usafiri wao kurudi nyumbani.

Blackwell alijitolea kusaini bendi hiyo katika lebo ya Island, na kuwalipa scheme ya kwanza ya gharama ya kurekodi albamu nyingine Jamaica.

Lakini bendi hiyo ilisikitika nyingi ya kazi zao zilifanyiwa mabadiliko ili kuvutia mashabiki wa kimaaifa.

Album hiyo haikufanya vyema na ilishuka katika chati za muziki nchini Marekani na Uingereza – lakini bado inakumbukwa kama moja ya muziki wa kale.

Baada ya kutengana na bendi, alianza kufanyia kazi albamu yake Blackheart Man, iliyojumuisha nyimbo za Dreamland ma Fighting Against Conviction, ambazo zilichangiwa na kifongo chake kifupi gerezani.

Aliendelea mbele na kutoa albamu zake tajika, ikiwemo ile ya mwaka 1981 ya Rock ‘n’ Groove na Bunny Wailer Sings The Wailers mwaka 1980, ambazo zilimfanya kuimarisha baadhi ya kazi za awali alizofanya akiwa kwenye bendi.

Miaka ya 1990, alishinda Tuzo ya Grammy ya Albamu bora ya reggae mara tatu – kila moja ya rekodi hizo zikiendeleza na kuhifadhi kumbukumbu ya Marley na bendi ya Wailers: Toleo la 1991 la Time Will Tell: A Tribute to Bob Marley, Crucial ya miaka 1995! Roots Classics, na utunzi wa miaka 1997 uliojumuisha nyota wote maarufu: Kwa heshima ya Bob Marley katika kumbukizi yake miaka 50.Bunny Wailer

Nyota huyu alijulikana kama mzee wa taifa wa reggae

“Nafarijika ninapotoa huduma kwa lengo la kuweka mbele muziki wa reggae na kuhakikisha unasalia kileleni,” aliambia gazeti la Washington Post mwaka 2016.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents