Technology

Habari nzuri kwa Bongo Fleva, Spotify kuzinduliwa Afrika Mashariki

Mtandao wa Spotify unatarajiwa kuzindua huduma zake katika masoko 85 mapya katika hatua ambayo itaipatia watu zaidi ya bilioni.

Tangazo hilo lilitolewa kupitia hafla iliyooneshwa mubashara kupitia mtandao ikiwajumuisha na Justin Bieber, Prince Harry na Meghan Markle.

Spotify pia imetangaza huduma mpya ya usajili wa ubora wa juu wa sauti na soko jipya la matangazo ya podcast.

Baadhi ya masoko mapya ya mtandao huo yako katika nchi zinazoendelea barani Asia, Afrika, Pacific na Caribbean.

“Masoko haya kwa pamoja yanawakilisha zaidi ya watu bilioni moja, nusu yao tayari wanatumia intaneti,” msemaji wa Spotify Alex Norstrom, alisema.

“Maeneo mengine tunayopeleka huduma zetu kama Bangladesh, Pakistan na Nigeria yana ukuaji wa haraka wa intaneti duniani,” aliongeza kusema.

Upanuzi wa awali wa mtandao huo nchini India, Urusi na Mashariki ya Kati tayari imewavutia mamilioni ya wafuatiliaji.

Masoko mapya ya Spotify yatakuwa Angola, Antigua na Barbuda, Armenia, Azabajani, Bahamas, Bangladesh, Barbados, Belize, Benin, Bhutan, Botswana, Brunei Darussalam, Burkina Faso, Burundi, Cabo Verde, Cambodia, Cameroon, Chad, Comoro, Côte d Ivoire, Curaçao, Djibouti, Dominica, Guinea ya Ikweta, Eswatini, Fiji, Gabon, Gambia, Georgia, Ghana, Grenada, Guinea, Guinea-Bissau, Guyana, Haiti, Jamaica, Kenya, Kiribati, Kyrgyzstan, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Lao, Lesotho , Liberia, Macau, Madagaska, Malawi, Maldives, Mali, Visiwa vya Marshall, Mauritania, Mauritius, Micronesia, Mongolia, Msumbiji, Namibia, Nauru, Nepal, Niger, Nigeria, Pakistan, Palau, Papua New Guinea, Rwanda, Samoa, San Marino , Sao Tome na Principe, Senegal, Shelisheli, Sierra Leone, Visiwa vya Solomon, Sri Lanka, Mtakatifu Kitts na Nevis, Mtakatifu Lucia, St Vincent na Grenadines, Suriname, Tanzania, Timor-Leste, Togo, Tonga, Trinidad na Tobago, Tuvalu, Uganda, Uzbekistan, Vanuatu, Zambia na Zimbabwe.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents