Haji Manara amejiuzulu nafasi yake Simba ? aandika imetosha

Kupitia ukurasa wake wa Instagram msemajiwa klabu ya @simbasctanzania @hajismanara ameandika ujumbe huu:-

“Hivi vitimbi mnavyonifanyia kila siku kisa Simba vishanichosha ,,,mwisho wa siku mtanitoa roho yangu kabla ya muda wangu…
Imetosha kwa sasa !!

Ubaya wote ni Haji lakini mafanikio ni yenu nyie Wakubwa..
Kila siku ni Haji Haji Haji..

Mkitoka kunisingizia hili mtatengeneza cinema nyingine kwangu,,tunashindwa kujua kila Mja Mungu kampa fungu lake,,,,inakuwaje Rizki ya umaarufu wa mwenzio iwahangaishe kiasi hcho?
Likinitokea baya pakuanzia mnapo.

Asanteni ndugu zangu na Mlipaji ni Mungu na ukweli utajulikana

IMETOSHA”

Related Articles

Back to top button