AfyaHabari

Hakuna karantini sababu ya Ebola – Museveni

Rais wa Uganda Yoweri Museveni ameondoa wasiwasi kwa umma uliodhani angetangaza hatua za karantini katika kudhibiti mlipuko wa ugonjwa wa Ebola.

Museveni akilihutubia taifa usiku wa kuamkia leo Alhamisi, kiongozi huyo amelezea kuwa hapana haja ya kuweka vizuizi kwa sababu ameona pana urahisi kudhibiti maambukizi ya Ebola ikilinganishwa na maambukizi ya virusi vya corona vinavyosababisha ugonjwa wa COVID-19.

Kiongozi huyo wa Uganda amesema kwenye hotuba yake kwamba kulingana na takwimu za wizara ya afya ni watu watano ndiyo wamethibitishwa kufariki kutokana na mlipuko wa Ebola tangu wizara hiyo ilipotangaza rasmi kwamba ugonjwa huo umegunduliwa nchini Uganda.

Waathirika kwa jumla ni 31 na kwamba kwa sasa idadi kubwa ya waathirika wamo katika wilaya tatu zilizo jirani.

Shirika la Afya Ulimwenguni WHO limesema ugonjwa wa Ebola ulionazia Sudan umeonesha kuwa hauambukizi kwa kasi na pia kiwango cha vifo ni cha chini tofauti na milipuko ya hapo awali uliotokea nchini Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ambapo karibu watu 2,300 walikufa mnamo mwaka 2018hadi mwaka 2020.

Huko nchini Uganda maambukizi ya hivi karibuni yalizuka katika wilaya ya Mubende katikati mwa Uganda, karibu kilomita 150 magharibi mwa mji mkuu Kampala na tangu wakati huo yameenea katika wilaya mbili zaidi.

Habari za kutokuwepo kwa hatua za karantini hata katika maeneo kulikogunduliwa wagonjwa wa ebola zimepokelewa kwa afueni kubwa na wananchi.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents