HabariSiasa

Hali tete Zimbabwe, mfumuko wa bei wafikia asilimia 200

Zimbabwe imetangaza mipango yake ya kuifanya dola ya kimarekani kuwa sarafu rasmi itakayotumika nchini humo kwa kipindi cha takriban miaka  mitano ijayo, pale taifa hilo linapojaribu kupambana na hali ya mfuumko wa bei unaozidi kupanda.

Waziri wa fedha wa Zimbabwe Nthuli Ncube alitoa tangazo hilo pale benki kuu ya nchi hiyo ilipozidisha kiwango cha riba maradufu kwa asli mia mia mbili ili kukabiliana na mfumko wa bei.

kupanda kwa gharama za maisha kumeonekana kuongezeka kutokana na tangazo la idara ya takwimu za kitaifa mwishoni mwa wiki kuwa mfumko wa bei umepanda kwa takriban asli mia 191.7 hapo Juni ikilinganishwa nai asli mia 131.7 ilivyorekodiwa hapo awali.

Zimbabwe ilianza kutumia dola ya kimarekani kwa pamoja na sarafu ya kwao hapo mwaka 2020, pale serikali ilipokuwa ikikabiliana na hali ngumu ya kiuchumi ilosababishwa na mlipuko wa Covid 19.

Sarafu ya Zimbabwe ambayo ilitolewa tena hapo mwaka 2019 baada ya mwongo mmoja imekuwa ikishuka thamani dhidi ya dola ya kimarekani, na kupelekea hali ya wasiwasi miongoni mwa wafanyakazi waliodai kulipwa kwa pesa za kigeni.

Gavana wa benki ya akiba ya Zimbabwe John Mangudya alilaumu kuongezeka kwa mfumko wa bei juu ya kutokwepo na imani wa soko kuwa serikali itaweza kumudu mfumo wa kutumia sarafu mbili.

Serikali ya rais Mnangagwa imekuwa ikihangaika kwa miaka kadhaa sasa kubadili hali ya kushuka kwa uchumi ulionza wakati wa enzi wa rais zamani Robert Mugabe, aliyepinduliwa hapo mwaka 2017.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents