Habari

Hali ya dharura yatangazwa New York, virusi vya Monkeypox vyashika kasi

Meya wa New York Eric Adams ,Jumatatu ametangaza hali ya dharura mjini humo hutokana na kuenea kwa virusi vya Monkeypox.

Kupitia taarifa iliyotolewa ikiwa kama amri ya kiutendaji, Adams amesema kwamba hatua hiyo itaimarisha juhudi zilizopo za kuhamasisha watu, kutoa chanjo pamoja na kutoa matibabu kwa watu wengi iwezekanavyo ili kuhakikisha kwamba mlipuko huo unadhibitwa kwa wakati.

Amri hiyo inampa Adams madaraka ya kusitisha baadhi ya sheria za mji na kuweka nyingine za muda, ili kudhibiti kuenea kwa maambukizi. Awali gavana wa jimbo hilo Kathy Hochul alikuwa ametangaza tahathari ya dharura ya jimbo akisema kwamba katika wiki 4 hadi 6 zijazo, serikali kuu itatoa chanjo 110,000 ili kuongeza kwenye 60,000 zilizopo tayari.

Kufikia Jumatatu, mji wa New York ulikuwa umeripoti kesi 1,472 za virusi vya Monkeypox kwa mujibu wa mtandao wa afya unaokusanya data mjini humo.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents