Bongo5 ExclusivesBurudaniHabariMahojiano

Hamisa Mobetto awapa makavu wanaomsema mtoto wake

Msanii na Mwanamitindo kutoka Tanzania Hamisa Mobetto ameamua kuwatolea uvivu watu wanaomsema mitandaoni kuhusu mtoto wake kuwa kunamkanganyiko kwenye upande wa baba yake.

Baada ya kuelezwa kuwa kuna uwezekano mkubwa Deeylan sio mtoto wa Diamond watu wamemjia juu kwa kuongea uongo kuwa yule mtoto wa Diamond kumbe sivyo.

Baada ya Mobetto kusema kuwa hakuna mama asiyemjua baba wa mtoto wake, wengi wamemuuliza kama alikuwa anamjua baba wa mtoto wake kwanini alidanganya ni mtoto wa Diamond hadi kumpeleka Diamond Mahakamani na Je pesa alizokuwa anampa Diamond ili amtunze mtoto itakuwaje.

Mbali na hivyo wengi wameenda mbali baada ya kuandika kuwa yule mtoto anafanana na Bilnass , Hamisa alijibu kuwa amejuana na Bilnass tayari ana mtoto.

Hamisa amewaonya watu waache kumuongelea mtoto wake mtandaoni kwani hawahusu.

Video nzima ipo katika akaunti yetu ya YouTube. Written and by @el_mando_tz shot and edited by @belege

Related Articles

Back to top button