Bongo5 ExclusivesBongo5 MakalaHabariMahojiano

Hananja: Watu wanaumizwa Makanisani kwa sababu ya visasi

Kufuatia sakata linaloendelea la Mchungaji Kimaro, Bongo5 tumezungumza na Mchungaji mstaafu wa Kanisa la KKKT Mchungaji Hananja ametoa maoni yake kuhusu sakata hilo.

Hananja ameeleza pia hata yeye aliwahi kusimamishwa mwaka mzima akiwa usharika wa Kigogo.

Akiongea na Bongo5 Mchungaji mstaafu wa Kanisa la KKKT ameeleza kuwa shida sio kusimamishwa shida ni kuwekwa wazi kosa lake nini??

Waliomsimamisha kimya kimya wanaweza kusababisha madhara kwa waumini wake. Amefananisha tukio hilo na movie akifafanua kuwa kuna bomu litalipuka muda sio mrefu.

Mchungaji Hananja ameshangazwa na kauli ambazo waumini wengi wakieleza huenda sababu ikawa ni kauli ya Kimaro aliyoitoa kuwa Makanisa mengine ni madalali.

Amesema kuwa kumhukumu mtu kwa kauli ile ni kosa kubwa kwani hata akienda mahakamani atakushinda kesi maana hakutaja jina la mtu, je kama na yeye amejijumuisha kwenye hao madalali.

Ameongeza kuwa sakata la Mchungaji Kimaro limeonyesha namna watu wamechukizwa na baadhi ya maamuzi yanayofanywa juu hivyo kuna uwanja mpana wa wao watoa maamuzi kujirekebisha haraka ili kuepusha madhara kwenye Kanisa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents