Bongo5 ExclusivesBurudaniHabariMahojiano

Hans Tone: WCB sio lolote sio chochote, msiwagope

Hayo ni maneno ya msanii chipukizi wa muziki wa Bongo Fleva Hans Tone juu ya lebo ya WCB ambaye ameonyesha chuki wazi wazi juu ya lebo hiyo kubwa ya muziki barani Afrika.

Hans Tone aliulizwa kuhusu tetesi zile zilizoenea kuwa atasainiwa katika lebo ya WCB na baadaye tukasikia ameachwa kutokana na utovu wa nidhamu.

Baada ya kuulizwa na wana habari Hans Tone alionyesha chuki kubwa na lebo hiyo huku akisema hawana lolote wale wala msiwaogope.

Kupitia katika kipindi cha Recap na Mando kipindi ambacho ni mahususi kwa ajili ya kukosea mambo mbalimbali kwenye tasnia ya muziki.

@el_mando_tz amejaribu kuliweka wazi na kumtahadharisha Hans Tone juu ya maneno anayoyaongea juu ya Lebo ambazo zinautangaza muziki wa Bongo Fleva na kuwashika vijana wengi mkono.

@el_mando_tz ameongeza kuwa hilo ni tatizo kwa wasanii wengi kukosa menejimenti na ndio maana wanashindwa kujua kipi cha kuongea mbele ya jamii na kipi cha kuacha na wasanii wengi wanapokosea huwa hawaambiwi ukweli.

Unahisi Hans Tone yupo sahihi kuongea maneno kama yale kuhusu lebo ambayo alitaka kusainiwa??

Related Articles

Back to top button