Burudani

Harmonize akutwa na Kizaazaa (Video)

Msanii Harmonize ameingia katika mzozo na waumini wa Dini ya Kiislamu huku wakimtaka afute mara moja maneno yake aliyoandika akimfananisha Mwenyezi Mungu na Mwanamke.

Kwa Mujibu wa kile alichoandika kupitia InstaStory yake Msanii huyo amesema imemchukua miaka 30 kugundua ya kuwa pengine Mungu ni Mwanamke kwa asilimia kubwa.

Mmoja ya waumini wa Dini ya Kiislamu Sheikh MasoudĀ  akizungumza na waandishi wa Habari amemtaka Harmonize kufuta haraka maandishi hayo akisema Mwenyezi Mungu kwa Mujibu wa imani ya dini hiyo, hafananishwi na Chochote.

“Huu ni msiba mkubwa kwa kijana wetu Harmonize “Anasema Sheikh Masoud kutoka moja ya kampuni ambazo zimekuwa zikipeleka mahujaji Makka

“Anapaswa afute haraka mno maneno haya” amesema sheikh Masoud

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

chanzo TanzaniaWeb.live

 

 

 

 

 

Imeandikwa na Mbanga B.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents