HabariSiasa

Hatma ya Ramaphosa ipo mikononi mwa Chama cha ANC

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa amesema hatma yake itatokana na uamuzi wa Halmashari Kuu ya Chama tawala (NEC) kutokana na tuhuma anazokabiliana nazo baada ya kukataa kujiuzulu.

Ramaphosa ambae pia atahudhuria mkutano huo uliopangwa kufanya leo hii, anakabiliana na tuhuma baada ya jopo la wataalam kubaini uwepo wa uwezekano wa kukiuka kiapo chake kazini kwa kuhusishwa na upatikanaji wa mamilioni ya dola katika shamba lake binafsi.

Kwa upande wake mara zote amekuwa akikana kuhusika na uovu wowote na hadi wakati huu hakuna mashtaka yaliofunguliwa dhidi yake.

Kikiso kazi cha chama tawala nchini Afrika kusini cha ANC kilikutana jana Jumapili mjini Johannesburg kujadili ripoti inayomweka matatani Rais Ramaphosa.


Related Articles

Back to top button