Michezo

Hatma ya Ronald Koeman ndani ya Barcelona mashakani 

Kwa mujibu wa ripoti ya ESPN, FC Barcelona wamewasiliana na Kocha wa Klabu ya Bayern Munich, Hansi Flick ili kuja kufundisha Camp Nou msimu ujao na hivyo kuzua mashaka mustakabali wa Ronald Koeman.

Flick, 56, mwezi Aprili aliweka wazi nia yake ya kuachana na Bayern mwishoni mwa msimu lakini ilielezwa kuwa alikuwa akikaribia kuchukua nafasi ya Joachim Low kama Kocha wa Ujeruman.

Kocha wa Barca, Ronald Koeman amesaliwa na mwaka mmoja katika kandarasi yake ndani ya Camp Nou lakini ESPN imeripoti kuwa kuna sitofahamu ndani ya bodi ya klabu hiyo juu ya maamuzi ya hatma ya baadaye ya Koeman.

Ralf Rangnick na Julian Nagelsmann ni miongoni mwa listi ambayo ina nafasi kubwa kuchukua mikoba kutoka kwa Ronald Koeman.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents