AfyaHabari

Hatua za dharura kuchukuliwa Ujerumani kukabiliana na homa ya Nyani

Mamlaka za afya nchini Ujerumani zimependekeza kuanza kuchukuliwa hatua za dharura kukabiliana na kusambaa kwa maradhi ya homa ya nyani, wakati Shirika la Afya Ulimwenguni likitangaza watu 250 kugunduliwa na virusi vya ugonjwa huo katika mataifa 16 ya Ulaya, Arabuni na Amerika.

Waziri wa Afya, Karl Lauterbach, amesema katika hatua hizi za awali za janga hilo, kunapaswa kuchukuliwa hatua kali. Waziri huyo amependekeza kuwa watu walioambukizwa virusi vya homa ya nyani wajitenge kwa siku 21 sawa na wale waliokutana na mwathirika.

Ujerumani imeagizia dozi 40,000 za chanjo ya ugonjwa huo hadi sasa, ambazo watachomwa wale waliokutana na mtu aliyethibitika kuambukizwa. Majimbo kadhaa ya Ujerumani yamethibitisha kuwepo kwa maambukizo ya ugonjwa huo. Shirika la Afya Ulimwenguni, WHO, linasema kuwa bado maradhi ya homa ya nyani yanaweza kudhibitika.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents