Hatupandi pikipiki kama Manara – Waziri Ndumbaro

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damasi Ndumbaro amesema ataongoza watanzania wote watakaojitokeza kushiriki maadhimisho ya miaka 60 ya uhuru kwa kupanda Mlima Kilimanjaro.

Dkt. Ndumbaro ameitoa kauli hiyo akiwa jijini Arusba ambapo amesema kuwa zoezi la kupanda mlima Kilimanjaro litahusisha kutembea kwa miguu na siyo kupanda pikipiki kama Haji Manara alivyofanya kwenye ‘Marathon’ mwaka jana.

Dkt. Ndumbaro amesisitiza kuwa kupanda mlima mrefu barani Afrika uliopo Tanzania ni uzalendo kwa kuwa mlima huo ni nembo moja wapo iliyoshirikishwa wakati wa uhuru ndio maana hata bendera ya Tanzania iliwekwa juu ya mlima huo.

Akitolea ufafanuzi suala la watalii wengine kupandishwa mlimani kwa kutumia usafiri wa ndege, Dk. Ndumbaro amesema fursa hiyo wanaziachia Taasisi binafsi kuchangamkia na kusisitiza kuwa serikali ikifanya hivyo ni kuwanyima watu wengine fursa ya kufanya kazi.

“Serikali kazi yetu ni kuhakikisha kwamba Mlima unafaa wakati wote kwa ajili ya Utalii. Suala la kuwekeza tunawaachia makampuni binafsi kuchangamkia fursa hiyo waangalie kama wanataka watalii wao wapande mlimani kwa kutumia ndege au usafiri mwingine.”

Ameongeza “Ila sisi tunapanda kileleni kwa miguu. Hatutapanda pikipiki kama Manara(akitania), kwanza njia ya mlimani usafiri wa pikipiki hauwezi kufika nao kileleni” Dkt. Ndumbaro.

BY: Fatuma Muna

Related Articles

Back to top button