Fahamu

Hawa ndio matajiri walioamua kusaidia jamii badala ya kuwapa watoto wao urithi wa mali hizo

Mwezi September ilikuwa zamu ya mtangazaji wa CNN Anderson Cooper ambaye anamiliki utajiri unaokadiriwa kuwa dola za kimarekani millioni 200, ambaye pia aliweka wazi kuwa hana mpango wa kuacha urithi wa mali zake kwa mtoto wake wa kiume ambaye sasa ana umri wa mwaka mmoja na nusu.

“Siamini katika kumuachia mtu kiasi kikubwa cha pesa, sina mapenzi na pesa lakini pia sina mpango wa kumuachia mwanangu wa kiume vitu kama dhahabu”.

Cooper’s na O’Neil’s ni sehemu ya mijadala ya matajiri wengi duniani juu ya hatma ya mirathi ya mali zao ambapo wanakumbuka visa maarufu vya matajiri ambao waliepuka kabisa kuwaachia warithi wao pesa.

Andrew Carnegie

Alipouza Kampuni yake ya Carnegie Steel mapema katika miaka ya 1900 mfanyabiashara huyu wa mkubwa wa chuma Raia wa Skotland na Marekani alipata kiasi dola millioni 480 ambacho kilikuwa kikubwa wakati huo. Na ilimfanya kuwa mtu tajiri zaidi duniani katika wakati wake.

Andrew Carnegie

Fedha hizi, hata hivyo, hazikwenda kwa warithi wake, Carnegie aliacha msemo maarufu uliojulikana kama “tajiri anayekufa kwa fedheha.” Msemo uliokuwa kwenye moja ya kitabu chake kilichojulikana kama ‘The Gospel of Wealth’.

Utajiri wa Carnegie ulitumika zaidi kufadhili ujenzi wa maktaba, taasisi za elimu pamoja na ufadili wa taasisi huko Marekani na Ulaya.

Chuck Feeney

Mwelekeo wa Andrew Carnegie ulikuwa wa ajabu kwa bilionea mwingine wa Marekani – huyu wa kisasa – Charles “Chuck” Feeney.

Mnamo 2020, mfanyabiashara huyo mwenye umri wa miaka 89 tayari alikuwa ametoa dola za Kimarekani bilioni 8 zilizokusanywa katika maisha yake yote kwenda kusaidia jamii kwa njia ya hisani (alikuwa mwanzilishi mwenza, katika miaka ya 1960, wa kampuni ya rejareja ya Duty Free Shoppers, au DFS).

Feeney alisema katika mahojiano kuwa “utajiri unaenda na kuwajibika”.

“Lazima watu wajieleze au wajisikie kuwajibika kutumia sehemu ya rasilimali zao kuboresha maisha ya wenzao, ama sivyo wataleta matatizo yasiyoweza kutatuliwa kwa vizazi vijavyo.”

Feeney anaishi maisha duni, bila nyumba za kifahari wala magari, ingawa mwaka 2012 aliiambia Forbes kuwa ametenga takriban dola milioni 2 kwa ajili ya kustaafu kwake na kwa mke wake.

Chuck

Kevin O’Leary

“Unamlaani mtoto unapoondoa hatari zote maishani mwake,” mfanyabiashara wa Canada Kevin O’Leary aliambia shirika la utangazaji la Marekani CNBC Septemba mwaka huu.

“Wengi wetu tunajua watoto walioharibika, matajiri ambao hawajali kutafuta kazi na hawana motisha ya kufanya hivyo kwa sababu maisha yao hayakuwa na hatari yoyote.”

Kwa sababu ya falsafa hii, O’Leary – mjasiriamali ambaye alianza utajiri wake na programu ya kompyuta na kuwa mtu mashuhuri wa televisheni nchini mwake kwa kuonekana katika programu kama Shark Thank (katika toleo la Kibrazili, Kujadiliana na Tubarões) – aliiambia CNBC kwamba alipopata utajiri pamoja na IPO yake ya kwanza (sadaka ya awali ya hisa), alianzisha hazina kwa ajili ya watoto wote katika familia yake.

Hazina hii inahakikisha, hata baada ya kifo cha O’Leary, kwamba wote wanalipwa gharama zao tangu kuzaliwa hadi chuo kikuu. “Baada ya hapo, hakuna mtu anayepata chochote.”

Yu Pengnian

Mwaka 2010, mfanyabiashara wa China Yu Pengnian, ambaye aliishi maisha ya unyenyekevu lakini akawa bilionea katika biashara ya majengo na hoteli, alitangaza kuwa tayari ametoa takriban dola bilioni 1.2 kwa ajili ya misaada ya kibinadamu.

Wakati Yu alipofariki mwaka wa 2015, akiwa na umri wa miaka 93, hakuacha chochote kwa warithi wake: wosia wake, kwa mujibu wa vyombo vya habari vya China, ulitaka pesa zote zilizobaki ziende kwa uhisani.

“Kama watoto wangu wana uwezo kuliko mimi, si lazima niwaachie pesa nyingi. Kama hawana uwezo, kuwaachia pesa nyingi kutawadhuru,” Yu alisema mwaka 2009, kwa mujibu wa gazeti la China Daily.

Alisema kuwa watoto wake walikubaliana na uamuzi wake huo wa kutumia seheu ya mali zake kwa jamii.

Katika wosia wake, pia aliiomba familia yake kutekeleza urithi wake kwa kuaboresho, masuala ya upasuaji wa mtoto wa jicho kwa watu wanaohitaji ufadhili wa masomo katika vyuo vikuu vya China.

kuchangia pesa katika maisha yao

Warren Buffet

Mabilionea wengine kutoka sekta mbalimbali – kutoka soko la fedha hadi teknolojia na sekta ya burudani – wamejitokeza hadharani kusema kwamba wana nia ya kuchangia sehemu kubwa ya utajiri wao wakati bado hai.

Majina kama vile Richard Branson, Warren Buffet, Michael Bloomberg, na Bill na Melinda Gates hushiriki katika The Giving Pledge, inayojieleza kama “dhamira ya watu tajiri zaidi na familia ulimwenguni kutoa utajiri wao mwingi kurudisha kwa jamii.”.

Huko Brazili, tukio la hivi karibuni lilimuhusisha David Vélez (mwanzilishi wa Nubank) na mke wake, Mariel Reyes. Katika barua iliyotolewa mnamo Agosti, wanandoa hao walisema wangetoa pesa zao kwa miradi ya kijamii katika Amerika ya Kusini sababu waliyosema ni kwamba: “kuna maana gani ya kufa na mali nyingi, wakati kiassi kidogo kinaweza kubadilisha sana safari ya mtu mwingine?” alihoji David.

Chanzo BBC.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents