Uncategorized
Hawa ndiyo wachezaji bora Afrika kwa mwaka 2018 akiwemo beki kisiki Koulibaly pamoja na golikipa wa Uganda

Fowadi matata kutokea nchini Misri, Mohamed Salah amefanikiwa kunyakuwa tuzo ya mchezi ji bora Afrika kwa mwaka 2018 huku Pierre-Emerick Aubameyang pamaoja na Sadio Mane wakitajwa kuwa fowadi matata wa Africa.

Katika nafasi ya viungo matata Thomas Partey, Naby Keita na Riyad Mahrez wametajwa kuwa ndio viungo bora wa mwaka 2018.

Na kwa upande wa mabeki, Eric Bailly, Serge Aurier, Medhi Benatia pamoja na Kalidou Koulibaly kutoka Senegal ambapo wametajwa kuwa wachezaji bora katika nafasi ya ulinzi.

Nafasi ya mlindalango imechukuliwa na kipa maarafu kutokea nchini Uganda Denis Onyango ambaye anaitumikia klabu ya Mamelodi Sundowns ya nchini South Africa.
