
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (@ChademaTz) Bara, @HecheJohn, amepokelewa kwa kishindo na hamasa kubwa leo, Jumatano, Februari 12, 2025, mjini Tarime.
Hii ni ziara yake ya kwanza Kanda ya Serengeti na Mkoa wa Mara tangu kuchaguliwa kwake.
Mapema leo amefanya mikutano ya hadhara na kuongea na wananchi wa Lamadi mkoani Simiyu na Bunda mkoani Mara, kabla ya kuhitimsha siku ya leo kwa kufanya mkutano wa hadhara katika jimbo la Tarime mjini.