Hekari 336 za Bangi zafyekwa Kondoa

Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama, imefyeka ekari 336 za mashamba ya bangi yaliyokuwa ndani ya hifadhi ya Ikome Wilaya ya Kondoa Mkoani Dodoma yakiwa yamechanganywa na mazao mengine halali ili kuficha shughuli hiyo haramu ambapo katika operesheni hiyo, kilo 148 za mirungi zilkamatwa.
Akiongea Wilayani Kondoa wakati wa utekelezaji wa operesheni hiyo, leo February 18, 2024 Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya, Aretas Lyimo amesema operesheni hiyo ni hatua kubwa katika vita dhidi ya dawa za kulevya “Hii ni operesheni kubwa ya kwanza kufanyika mkoani Dodoma,
Ikionyesha wazi kuwa kilimo cha bangi kimeanza kuenea katika baadhi ya maeneo ya Mkoa huu, tutaendelea kuchukua hatua kali kuhakikisha kuwa uzalishaji, biashara na matumizi ya dawa za kulevya vinadhibitiwa kwa nguvu zote” Katika hatua nyingine amesema Kanda ya Ziwa, hususan Wilaya ya Rorya Mara, ekari 24 za mashamba ya bangi ziliteketezwa, huku Watuhumiwa sita wakikamatwa, Kanda ya Pwani, inayojumuisha Mikoa ya Mtwara, Pwani na Ruvuma, zilikamatwa kilogramu 322.201 za bangi, kete nane na misokoto 216 ya bangi, pia ekari nne za mashamba ya bangi ziliharibiwa na Watuhumiwa nane walikamatwa, Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, hususan Mkoa wa Mbeya kilogramu 21 za bangi zilikamatwa huku Watuhumiwa 11 wakishikiliwa.