Habari

Helikopta ya kijeshi ya Uganda yaanguka mashariki mwa DRC, Upelelezi umeanza

Jeshi la Uganda limeanza uchunguzi kuhusu ajali ya ndege aina ya helikopta ya jeshi iliyoanguka mashariki mwa Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Congo Jumanne.

Msemaji wa jeshi la Uganda (UPDF), Brigadia Jenerali Felix Kulaigye anasema mkuu wa majeshi ameteua wajumbe kumi na wawili kuanza kufanya kazi hiyo ya uchunguzi leo.

Helikopta hiyo ilianguka muda mfupi baada ya kuwasilisha chakula na bidhaa nyingine muhimu kwa wanajeshi ambao kwa sasa wanapigana sambamba na vikosi vya Congo dhidi ya waasi wa Uganda, wa Allied Democratic Force (ADF).

Imeripotiwa kuwa sehemu ya nyuma ya ndege hiyo ilikwama kwenye mti, na kusababisha kuzunguka na hatimaye kuanguka.

Idadi ya waliofariki na majeruhi katika ajali hiyo bado haijatangazwa.

Kulaigye anasema kwamba taarifa itapatikana baada ya ndugu zao kufahamishwa, lakini akaongeza kwamba majeruhi wamepelekwa kwenye hospitali ya kijeshi iliyopo Bomb kilomita 30 kutoka mji mkuu Kampala.

Wanajeshi wawili hatahivyo wameweza kunusurika bila kujeruhiwa baada ya kuruka nje ya helikopta.

Ajali ya hivi karibuni inakuja siku chache baada ya helikopta nyingine ya kijeshi kutua kwenye nyumba ya mwanamke mwingine mkongwe katika mji wa magharibi wa Fort Portal.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents