Fahamu

Helikopta ya kwanza isiyo na rubani yafanikiwa kupaa sayari ya Mars (+ Video)

Shirika la masuala ya anga za juu la Marekani (NASA) limefanikiwa kurusha ndege ndogo aina ya helikopta katika sayari ya Mars.

Ndege hiyo isiyo na rubani, kwa jina la Ingenuity , ilipaa katika sayari ya Mars kwa chini ya dakika moja lakini Nasa inasherehekea kile hatua kubwa ya kuwa ndege isiyo na rubani inayodhibitiwa duniani iliyofanikiwa kupaa katika sayari nyengine.

Uthibitisho ulijiri kupitia setlaiti iliyopo Mars ambayo ilituma data ya ndege hiyo duniani.

Shirika hilo limeahidi kutuma ndege nyengine katika siku zijazo.

Ingenuity itasukumwa iruke juu zaidi huku wahandisi wakijaribu kupima viwango vya teknolojia hiyo.

Ndege hiyo ilibebwa hadi Mars na gari maalum aina ya roboti liitwalo Perseverance Rover na kutua katika kreta ya ya Jezero katika sayari nyekundu mwezi Februari.

 

Graphic

”Tunaweza kusema kwmba binadamu wamerusha ndege katika sayari nyengine”, alisema MiMi Aung, meneja wa mradi wa Ingenuity katika maabara ya Nasa huko Pasadena California.

”Tumezungumza kwa muda mrefu kuhusu Ndugu wawili wa Wright katika sayari ya Mars na hivi ndivyo ilivyo”.

Walikuwa wakizungumzia Wilbur na Orville Wright waliohusika na kurusha ndege ya kwanza hapa duniani mwaka 1903.

Ingenuity pia inabeba kipande kidogo cha kitambaa katika mojawapo ya mabawa yake kwa jina Flyer 1, ndege ilioweka historia katika eneo la Kitty Hawk, huko North Carolina zaidi ya miaka 117 iliopita.

ShadowKulikuwa na shangwe na nderemo katika kituo hicho cha JPL baada ya picha za kwanza za ndege kuwasili duniani. Nyuma yake , Mimi Aung alisikika akisema , ”ni kweli”!

Na kufuatia makofi yaliopigwa na wafanyakazi wenzake, alikatakata hotuba iliokuwa imeandikwa tayari iwapo ndege hiyo ingefeli .

Maonyesho hayo yalipelekea ndege hiyo kuruka urefu wa mita tatu kukaa angani na baadaye kutua .

Ilifanikiwa kuruka angani kwa sekunde 40 kutoka kupaa hadi kutua kwake.

Kuruka angani katika sayari nyekundu sio rahisi . Hali ya hewa ni nyepesi , ikiwa ni asilimia moja pekee ya uzito uliopo duniani.

Hatua hiyo inayapatia mabawa ya ndege hali ngumu kupaa angani. Kuna usaidizi kutoka kwa mvuto uliopo chini ya Mars, lakini inachukua kazi kubwa kuweza kuondoka ardhini.

Ingenuity hivyo ilitengezwa kwa uzito mwepesi na kupewa kasi kubwa ya kupeperusha mapanga yake. Ndege hiyo inaongozwa duniani ambako ni umbali wa kilomita takribani milioni 300.

Selfie of helicopter and rover

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents