HabariMichezo

Hersi apitishwa Urais Yanga

Leo Jumamosi June 11, 2022, Kamati ya Uchaguzi Yanga SC imetaja orodha ya Wagombea waliopitishwa kugombea nafasi mbalimbali katika Uongozi wa Yanga SC ambapo Injinia Hersi Ally Said @caamil_88 amekuwa Mgombea pekee aliyepitishwa kwa kukudhi vigezo vya kikatiba na Kanuni kuwania nafasi ya Urais katika Klabu ya Yanga na Katika nafasi ya makamu wa Rais yamepita majina mawili ya Arafat Haji na Suma Mwaitenda.

Hata hivyo katika nafasi ya ujumbe wa kamati ya Utendaji ambapo kwa mujibu wa katiba ya Yanga itakuwa na wajumbe watano yamepitishwa majina 22 kati ya 27 likiwemo jina la Mbunge wa Manonga Seif Khamisi Gulamali.

Majina matano yaliokatwa kwa kigezo cha kushindwa kukidhi baadhi ya vigezo vya kikatiba ni pamoja na Ayubu Shaibu Nyenzi, Sindilo Lyimo, Mustapha Salumu Himba, Kara Remtullah na Tobias Bosco Lingalangala.

Related Articles

Back to top button