FahamuHabari

Hezbollah yasema itazidisha vita na Israel baada ya kiongozi wa Hamas kuuawa

Kundi la wanamgambo wa Hezbollah nchini Lebanon limesema Ijumaa kuwa linaelekea katika awamu mpya na ya ya kuzidisha vita vyake zaidi dhidi ya Israel huku Iran ikisema “roho ya upinzani itaimarishwa” baada ya kuuawa kwa kiongozi wa Hamas Yahya Sinwar.

Sinwar, ambaye alikuwa mpangaji mkuu wa shambulio la Oktoba 7, 2023, ambalo lilianzisha vita vya Gaza, aliuawa wakati wa operesheni ya wanajeshi wa Israel katika eneo la Wapalestina siku ya Jumatano, likiwa ni tukio muhimu katika mzozo huo wa mwaka mzima.

Viongozi wa nchi za Magharibi wamesema kifo chake kilitoa fursa kwa mzozo huo kumalizika, lakini Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema vita hivyo vitaendelea hadi mateka waliotekwa na wanamgambo wa Hamas warejeshwe.

“Leo tumepata matokeo. Leo uovu umepata pigo lakini kazi yetu bado haijakamilika,” Netanyahu alisema katika taarifa ya video iliyorekodiwa baada ya kifo cha Sinwar kuthibitishwa Alhamisi.

“Kwa familia pendwa za mateka, ninasema: Huu ni wakati muhimu katika vita. Tutaendelea kwa nguvu zote hadi wapendwa wako wote, wapendwa wetu, wawe nyumbani.”

Sinwar, ambaye alitajwa kama kiongozi mkuu wa Hamas kufuatia mauaji ya mkuu wa kisiasa Ismail Haniyeh mjini Tehran mwezi Julai, aliaminika kuwa alikuwa amejificha kwenye mahandaki ambayo Hamas imejenga chini ya Gaza katika kipindi cha miongo miwili iliyopita.

Aliuawa wakati wa makabiliano ya bunduki kusini mwa Gaza siku ya Jumatano na wanajeshi wa Israel ambao awali hawakujua kuwa wamemkamata adui nambari moja wa nchi yao, maafisa wa Israel walisema.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents