Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro namba 12 duniani (+ Video)

Mbuga ya wanyama ya Serengeti nchini Tanzania imechaguliwa kuwa mshindi wa vivutio vya utalii duniani na kampuni ya Tripadvisor.

Tuzo hizo hutolewa na kampuni hiyo inayoshushughulika na kutoa mrejesho wa mahoteli na vivutio mbalimbali duniani.

Hifadhi tatu nchini Tanzania zimeibuka kidedea kati ya hifadhi 25 zilizotajwa kwenye tuzo hizo Serengeti ikishika nafasi ya kwanza duniani Hifadhi ya Masai Mara ya nchini Kenya imeshika nafasi ya tatu huku mbuga ya wanyama Tarangire ikishika nafasi ya 14 na hifadhi ya Mlima Kilimanjaro ikishika nafasi ya 12.

Waziri wa Mali Asili na utalii nchini Tanzania Dkt Damas Ndumbaro amesema tuzo hiyo ni yenye umuhimu mkubwa kwa Serengeti

Serengeti pekee kwa mwaka hupokea wastani wa wageni laki tatu na nusu hadi laki tano ambao huja kushudia maajabu yaliyoko kwenye eneo hili ambalo ni urithi wa dunia ikiwa na na ukubwa wa kilomita za mraba 14750 kila mwaka hushuhudia mamilioni nyumbu ambao wanahama kutoka hifadhi Masai mara nchini Kenya ambayo nayo kwenye tuzo hizi imeshika nafasi ya tatu.

Bofya hapa chini Kutazama.

https://www.instagram.com/tv/CMB8qkYB3k_/

Related Articles

Back to top button