Umbea

Hii kali: Alaghai kwa kujiita Miss Tanzania na kuiwakilisha Tanzania Miss Africa USA


Well bongo5.com today kupitia segment yetu ya gossip tunawaletea habari ya mwanadada Maggie Munthali, ambaye aliiwakilisha Tanzania Jumamosi iliyopita katika mashindano ya kumtafuta Miss Afrika USA huko Washington DC…lakini cha kushangaza ni kwamba Maggie hajawahi hata siku moja kushiriki katika kinyang’anyiro cha Miss Tanzania, sasa swali ambalo watu wengi wanajiuliza, ni je aliipata wapi nafasi hii?

Watanzania wamesikitishwa sana na ulaghai wa aina hii, kwani washiriki wote walioshiriki walikuwa ni warembo walioshinda mataji katika nchi zao walizotoka….au warembo walioshinda mataji ndani ya USA kwa kuziwakilisha nchi zao, sasa huyu dada hajawahi kushiriki Miss Tanzania na kushinda Tanzania wala hajawahi kushiriki mashindano ya kumtafuta Miss Tanzania wakati yupo USA..imekuwaje mpaka akavaa taji la Miss Tanzania na kuiwakiliksha nchi yetu.

Kumekua na gumzo hasa kwa Watanzania wanaoishi Marekani na kujiuliza ni nani hasa mwenye makosa? Ama kuna mpango ambao ulitengenzwa hasa lawama zao zikienda kwa mamlaka ya Miss Tanzania au hawakuwa na taarifa kuhusu mashindano haya.

Bongo5 imepata taarifa kutoka kwa KATHLEEN BENSON, Mtanzania anayeishi Marekani tunamnukuu alichotutumia, anasema hivi “Hashim Lundenga anaelewa swala hili? Je Lundenga alimruhusu huyu dada kuiwakilisha Tanzania nje ya nchi? Kama alimruhusu alitumia vigezo gani kumchagua? Tunapenda kuwakilisha na tunamsapoti Mtanzania yeyote anayetuwakilisha nje ya nchi lakini apitie katika njia zilizosahihi”. Anamwelezea Maggie Munthali kuwa hajawahi kushiriki mashindano yoyote ya kutafuta Miss Tanzania ndani na nje ya nchi.

Aliendelea na kusema “kama tumekosea alishawahi kushiriki basi bwana Lundenga tunaomba atuwekee wazi picha zake akiwa katika mashindano ya kumtafuta Miss Tanzania popote pale ndani na nje….na tunaomba ajaribu kutuambia kama ni kweli alishinda na kutwaa taji hilo?”

“Wapo ma miss wengi ambao wanafanya kazi kubwa sana kuweza kufikia kuitwa Miss, wamevuja jasho kupitia vikwazo hadi kushinda na kuiwakirisha nchi vyema….tunaomba mtu anapoamua kuibeba bendera ya nchi asiwe mtu wa kufoji…..huu ni ulaghai wa mtu kujiita Miss Tanzania wakati hajawahi kuwa hivyo. Tunaomba pia swala hili mheshimiwa Lundenga kama sio la halali basi lifikishwe kwa waandaaji wa Miss africa USA kwani inawezekana kabisa wamerubuniwa, habari hizi pia tutazipeleka wizara ya mambo ya nje kwani huwezi kuiwakilisha nchi pasipo uhalali..! Ahsante…..mungu ibariki Tanzania”.

Hayo ndio maelezo ya dada Kathleen aliyetutumia ujumbe huo akieleza dukuduku lake kinagaubaga kwa Watanzania ili tuweze kusonga mbele katika nafasi ambazo tunazipata na tupunguze udanganyifu katika mambo yetu muhimu. Kwa hali ya kawaida hizi taarifa zikifika sehemu husika kama Miss Afrika USA tunaweza tukafungiwa kushiriki na kukosa fursa kwa ajili ya ndugu,jamaa na marafiki zetu.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents