Habari

Hii ndio sababu kipindi cha TV cha Rose Ndauka kiliishia hewani

Pamoja na kuwa muigizaji wa filamu, Rose Ndauka ni mtangazaji wa TV.

1074697_560696530695496_181432518_o

Miaka miwili iliyopita alianzisha kipindi chake cha TV kilichopewa jina la ‘Family Talk Show’. Kupitia kampuni yake, muigizaji huyo alianza kurekodi episodes kadhaa za show hiyo ili zianze kuruka kwenye TV.

Hata hivyo kipindi hicho hakijawahi kuonekana na ni kama kiliishia hewani. “Kipindi changu.. niliibiwa vitu vyote ofisini lakini ndoto yangu ya utangazaji iko pale pale,” Rose aliiambia Kabali ya EFM.

901141_394322987332852_1456161880_o
Mwanzoni mwa mwaka 2013, Rose Ndauka alianza kushoot kipindi chake cha TV ambacho hata hivyo kiliishia hewani

March 23, 2013 kupitia akaunti yake ya Facebook, Rose aliweka picha akiwa studio akirekodi kipindi hicho na kuandika: MWAKA HALOOO TZ WELCOME TO THE FAMILY TALK SHOW FROM KIKOI TANZANIA LIMITED AND THAT IS OUR HOST>>> ROSE DONATUS NDAUKA, GET READY TO SEE NEW ROSE NDAUKA.”

Hivi karibuni mrembo huyo alianzisha jarida la mtandaoni liitwalo Rozzie Magazine na hivyo kuashiria kuwa ameamua kubadilisha muelekeo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents