Msanii wa muziki wa Hip Hop kutoka Kenya, @Gidi_Kocha ameachia ngoma mpya (Diss Track) akimchana Rapper mwenzake kutoka Kenya Khaligraph Jones baada ya kauli yake ya kuwabeza Ma-Rappers kutoka Tanzania. Bofya hapa chini kusikiliza ngoma hiyo.
Kwenye ngoma hiyo ya ‘Paragraph Jones’ @Gidi_Kocha amesikika akisema Wasanii wa Hip Hop Bongo ni wakali na wakubwa sana hapa Afrika Mashariki kuliko Nchi yeyote ile, Hivyo amewakosea sana ma-rappers wa Tanzania.