Hiki Chuma kinaenda kuleta maafa Msimbazi
Mshambuliaji wa Singida Black Stars, Ismail Mgunda yupo katika mazungumzo na Simba ili kujiunga na kikosi hicho msimu ujao. Mgunda aliyemaliza na mabao sita ya Ligi Kuu, amefuatwa na viongozi wa Simba ili akaichezee, ikielezwa mazungumzo yanaendelea Singida ikiwa tayari kumuachia.
SIMBA imefungua mazungumzo ya kuipata saini ya mshambuliaji wa Ihefu FC hivi sasa ikiitwa Singida Black Stars, Ismail Mgunda anayewaniwa vikali na Red Devils ya nchini Ghana.
Mgunda ndiye alikuwa anaunda safu nzuri ya ushambuliaji pamoja na Elvis Rupia katika kikosi cha Singida Black Stars katika msimu huu.
Simba imepanga kukiboresha kikosi chao, ili kifanye vema katika msimu huu, kati ya sehemu ambazo imepanga kuziboresha ni safu ya ushambuliaji.
Kwa mujibu wa taarifa ambazo imezipata Championi Ijumaa, Simba ipo katika mazungumzo ya mwishoni na mshambuliaji huyo, ambaye yupo katika rada za kusajiliwa na Red Devils inayoshiriki Ligi Kuu ya Ghana.