Bongo5 ExclusivesBongo5 MakalaFahamuHabari

Hili ndio Jumba la CIA lenye siri kubwa duniani, silaha za kila aina zimehifadhiwa humu

Labda ni jumba la makumbusho lisilo la kawaida – na la kipekee – ulimwenguni, lililojaa vitu vya sanaa ambavyo vimeunda historia.

Lakini milango yake imefungwa kwa umma.

Ni sehemu pekee ambayo mgeni anaweza kuona bunduki iliyopatikana na Osama bin Laden alipouawa, karibu na koti la ngozi la Saddam Hussein.

Karibu kwenye jumba la makumbusho la siri la CIA.

Ukiwa ndani ya makao makuu ya shirika la kijasusi la Marekani huko Langley, Virginia, mkusanyiko wa vitu hivyo  umekarabatiwa hivi punde ili kuadhimisha mwaka wa 75 wa shirika hilo.

Kikundi kidogo cha waandishi wa habari, ikiwa ni pamoja na BBC, walipewa ufikiaji wa kipekee, ingawa waliandamana na  usalama tena kwa karibu kila walipokwenda.

Miongoni mwa sanaa 600 zinazoonyeshwa ni aina ya vifaa vya kijasusi vya vita baridi unavyoweza kutarajia – ‘panya waliyekufa’ ambamo ujumbe unaweza kufichwa, kamera ya siri ndani ya pakiti ya sigara, njiwa mwenye kamera yake ya kijasusi na hata glasi ya Martini inayolipuka.

Lakini pia kuna maelezo juu ya baadhi ya operesheni maarufu zaidi za Shirika la Ujasusi la Marekani (CIA) na hata za hivi karibuni.

Kwenye onyesho ni mfano wa ukubwa wa kiwanja ambamo Osama bin Laden aligunduliwa nchini Pakistan.

Rais Obama alionyeshwa mfano huo kabla ya kuidhinisha uvamizi uliomuua kiongozi wa al-Qaeda mwaka wa 2011.

‘’Kuweza kuona mambo katika mfumo wa 3D kwa kweli kuliwasaidia watunga sera…na pia kusaidia waendeshaji wetu kupanga misheni,’’ anaelezea Robert Z Byer, mkurugenzi wa makumbusho ambaye alitoa ziara.

Tarehe 30 Julai mwaka huu kombora la Marekani lilipiga eneo jingine, safari hii katika mji mkuu wa Afghanistan Kabul.

Aliyelengwa alikuwa kiongozi mpya wa al-Qaeda, Ayman al-Zawahiri.

Na maonyesho ya hivi majuzi zaidi, ambayo yametolewa tu, ni mfano wa kiwanja kilichotumiwa kumjulisha Rais Biden mnamo Julai 1, 2022 juu ya misheni iliyopendekezwa.

Zawahiri alivamiwa akiwa kwenye roshani baada ya jumuiya ya kijasusi ya Marekani kutumia miezi kadhaa kuchunguza mienendo yake.

‘’Inazungumzia jinsi maafisa wa kukabiliana na ugaidi wanavyoangalia mtindo wa maisha ya walengwa,’’ anaelezea Bw Byer.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents