
“Katika miaka hii 67 ya kufanya uchaguzi, mifumo yetu ya uchaguzi imepitia mabadiliko mengi sana, sheria zetu za uchaguzi zimefanyiwa marekebisho zimetungwa upya, katiba zetu zimebadilishwa , kwa kiasi kikubwa katika hii miaka 67 tumejifunza mengi, leo tunapozungumza tunategemea nini hasa? Swali hili ni muhimu kwasababu ya matukio ambayo tumeyaona katika chaguzi tulizozifanya katika takribani miaka mitano tangu tulipofanya uchaguzi mkuu wa 2015. Ninazungumzia uchaguzi wa mitaa na vijiji wa mwaka 2019, Uchaguzi Mkuu wa Marais, madiwani na wabunge wa mwaka 2020 na uchaguzi wa mitaa na vijiji uliofanyika Novemba 2024. Chaguzi hizi tatu zinatupa sababu ya kujiuliza uchaguzi mkuu wa mwaka huu utakuaje?”- Lissu.
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Taifa, Tundu Lissu akizungumza na wanahabari Makao Makuu ya chama hicho mkoani Dar es Salaam siku ya Jumatano Februari 12, 2025.