Fahamu

Historia ya kijana aliyetupwa na wazazi wake jalalani sasa hivi ni bilionea (+ Video)

Kwa mujibu wa orodha ya hivi karibuni ya watu waliopata mafanikio na kuwa watu bora , kampuni ya Freddie Figgers cina ina thamani ya dola milioni 62.

Alipokuwa mtoto mchanga, Figgers alitupwa karibu na pipa la takataka katika eneo la vijijini la Florida nchini Marekani

“Watoto walikuwa wakimcheka, walikuwa wakimuita ‘mtoto takataka’, walimwambia ‘hakuna mtu anayeku[penda wewe…wewe ni mchafu ‘.

”Nakumbuka nyakati fulani nilipokuwa nikitoka ndani ya basi la shule watoto walikuwa wananivuta na kunitupa katika [pipa la takatakana kunicheka , “alimwambia Jo Fidgen katika mahojiano na kipindi cha BBC ” BBC Outlook. “

“Ilifika wakati ikambidi baba yangu awe ananisubiri kwenye kituo cha basin a kunisindikiza hadi nyumba, na watoto walinisumbua hata zaidi, huku wakinikejeli : ‘Ha ha! Hebu tazama mwanaume huyo mzee mwenye takataka .’

Baba yake Figgers, Nathan, alikuwa na umri wa miaka 74 na mama yake, Betty May, 66 walipomuokota.

Walikuw ana watoto wao, na walikuwa wamewachukua watoto wengine kumi na wawili wa kulea kwa miaka kadhaa- wengi wao wakati wazazi wao walipokuwa gerezani – na walikuwa wamepanga kuacha kuwachukua watot zaidi wa kule kwasababu walikuwa wanazeeka .

Lakini ghafla Freddie akawasili.

Hakuwa na mtu yeyote aliyemtaka, kwahiyo wakamuasilina kumkuza kama mtoto wao.

Wakati Freddie alipoanza kuuliza maswali , Nathan aliyafananisha na historia yake.

“Alisema . ‘Ninakwenda kukwambia ukweli bila kukuficha, mama yako mzazi alikutelekeza . Na mimi na Betty hatukutaka kukupeleka katika kituo cha kuwatunza watoto, tulikuasili. Nilijihisi kama takataka nakumbuka akinishika mabega na kuniambia , ‘Usikubali hilo likuudhi .’

Betty May y Nathan Figgers
Betty May na Nathan Figgers walikuwa wameamua kutomchukua mtoto mwingine wa kulea tena…wakati Ferddie alipowasili

” Wazazi wangu walinipa upendo ambao yeyote angetaka apewe. Walinifanyia kila kitu. Sikuwahi kuhisi haja ya kuitafuta familia yangu ya damu kwasababu baba yangu na mama yangu , Betty wangu na Nathan wangu, walikuwa kila kitu kwangu . Niliwapenda. “

“Ni watu wazuri. Walinifunza kuwa na maadili, kufanya jambo sahihi, kutosahau nilipotoka. Nilimuona baba yangu kila mara akiwasaidia watu, akisimama njiani kuwasaidia watu wasiojulikana, akiwalisha watu wasio na makazi …

“Alikuwa mtu mwema sana na ninataka kuwa kama yeye .”

Kuanzia katika takataka hadi kuwa wa thamani

Nathan alikuwa na kazi mbili, kazi ya ukarabati wa nyumba, Betty May alikuwa mfanyakazi wa kiwandani, na ingawa hawakuwa na pesa nyingi wakati Freddie alipokuwa na umri wa miaka 9 walimnunulia zawadi ambayo ilibadili kila kitu maishani mwake : kpmpyuta aina ya Macintosh … iliyopasuka.

“katika siku za wikendi nilikuwa ninakwenda na baba yangu kufanya kile ambacho tulikiita ‘kuendesha takataka ‘, kutembea tukizurura kwenye nyumba za majirani kutafuta vitu ambavyo watu wamevitupa, kama msemo usemao : Kile ambacho kwa mtu mmoja ni takataka, kwa mwingine ni cha thamani . “

“Nimekuwa wkati wote nikifurahishwa na kushangazwa sana na kpmpyuta. Nilikuwa na ndoto ya kpmpyuta ya Gateway lakini hatukuweza kuinunua.”

Wakati ule, baba yake alimchukua katika duka la bidhaa zilizotumiwa ambako alimshawishi muuzaji kuwauzia kompyuta iliyoharibika, ambapo waliinunua kwa dola 24.

Freddie Figgers con su computadora
 

“Nilifurahi. Kwasababu ilikuwa haiwaki, Niliichukua kando nikagundua kuwa ilikuwa imepasuka na kila kitu kilifanyika kwa urahisi. Baba yangu alifanya kazi ya ukarabati wa bidhaa na na alikuwa na vitu vingi kama vile kifaa cha kuchomelea, redio na saa …”

“Nilichukua sehemu ya saa ya redio na kuvifunga pamoja na baada ya kujaribu mara 50 hatimae nikapata kompyuta inafanya kazi. Ni wakati ule ambapo nilifahamu ni nini ninachotaka kukifanya maishani mwango .”

“Kompyuta ilinifutia maumivu yote ya kudhalilishwa. Wakati nilipokuwa ninadhalilishwa shuleni , nilikuwa ninafikiria tu kwenda nyumbani kucheza na kompyuta yangu.

“Nilijifunza alama ya siri nilipokuwa na umri wa miaka 10 au 11 na nikaanza kuandika programu za kimsingi. Hapo ndipo nilipoanza kusonga mbele .”

Mshahara uliotokana na kazi niipendayo

Muda mfupi baada ya kujifunza lugha ya kompyuta , alipata kazi yake ya kwanza. Akiwa na umri wa miaka 12.

“Nilikuwa nikienda katika mpango wa masomo ya baada ya shule na kuutumia muda wangu kujifunza katika maabara ya kompyuta .”

“Hapakuwa na mtaalamu wa kompyuta kwahiyo wakati kmpyuta ilipokuwa inazima , walikuwa wanachomoa waya wake wa umeme na kuiunganisha na nyingine iliyoharibika . Nilikuwa ninachukua sehemu zilizoharibika na kuziunganisha na sehemu ambazo hazijaharibika za kompyuta nyingine.”

Wakati huo , mkurugenzi mkuu wa mpango huo alikuwa ni Meya wa jiji la Quincy, na pale alipoona kile ambacho Freddie alikifanya, alishangaa sana, na kuwaomba wazazi wake ruhusa na kumpeleka katika makao makuu ya jiji.

Freddie Figgers niño

Walikuwa na makumi kadhaa ya kompyuta zilizopasuka pale na Ferddie alijitolea kuzitengeneza kwa kwenda pale kila siku baada ya shule . Walimlipa dola 12 kwa saa, lakini ” lengo halikuwa hasa pesa—nilifurahia!”

Miaka mitatu baadae, alipokuwa na umri wa miaka 15 na akiwa bado anafanya kazi katika manispaa , kampuni ilitoa mpango wa kufuatilia kiwango mita za maji kwa dola za kimarekani 600,000. Maafisa walifikiria kuwa liliwa ni wazo zuri kumpatia jukumu Ferddie kuusimamia, ambaye alibuni mpango waliouhitaji kwa mshahara ule ule waliokuwa wakimlipa.

Ni wakati huo ambapo alifanya uamuzi .

“Wakati ule shule ilikuwa imenichosha kwahiyo nikaamua kuiacha na kuanza biashara yangu mwenyewe, ingawa wazazi wangu hawakukubaliana na mimi .”

Bofya hapa kutazama zaidi.

https://www.instagram.com/tv/CLymi2wBPnL/

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents