Historia ya Nyerere kurithishwa kwa vitendo

Shirika la Hifadhi ya Taifa Tanzania (TANAPA) kwa kushirikuana na Kumbukizi ya Nyumba ya Mwl. Nyerere inatarajia kufanya kampeni ya Kurithisha historia kwa Vitendo.

Hayo yamewekwa wazi na Mhifadhi Mwandamizi wa Kumbukizi wa Nyumba ya Mwl. Nyerere, Neema Mbwana leo Oktoba 11 wakati akizungumza na wanahabari.

Bi Neema amesema historia ikifundishwa kwa vitendo hasa kwa kufika katika Nyumba hiyo ya Kumbukumbu ya Mwl. Nyerere iliyopo Magomeni Jijini Dar es salaam itasaidia wanafunzi kuelewa namna Uhuru wa nchi yao ulivyopiganiwa.

Akizungumzia kuhusu uendeshwaji wa Kampeni hiyo yenye lengo la kudumu kwa takribani miezi mitatu, Bi. Neema amesema mpaka sasa kuna mwitikio wa shule zaidi ya 120 kwa Dar es salaam na matarajio ni kufikia shule zote za Sekondari na Msingi, binafsi na serikali.

Kampeni ya Kurithi Historia kutoka kwa Mwalimu Nyerere imeanzishwa Oktoba 1 ikiwa ni mwezi wa Kumbukumbu ya Kifo cha Hayati Mwl. Julius Nyerere na Kilele chake kinatarajia kuwa Disemba 3, 2021.

Related Articles

Back to top button