Hizi ndio sababu za Instagram, faceboo na Whatsapp kushindwa kufanya kazi kwa masaa 6

Huduma za mitandao ya kijamii Facebook, WhatsApp na Instagram zimerudishwa baada ya kukatika kwa karibu masaa sita, Facebook imesema.

Kampuni hiyo inasema sababu ilikuwa mabadiliko yaliyofeli ya mfumo. Huduma zote tatu zinamilikiwa na Facebook na hazikuweza kupatikana kwenye wavuti au kwenye programu za simu za mkononi.

Downdetector, ambayo inafuatilia kukatika kwa huduma za mitandao ya kijamii ilisema ni hitilafu kubwa zaidi kuwahi kutokea, na ripoti milioni 10,6 za matatizo kutoka kwa wateja kote ulimwenguni.

 

Huduma zilikatika saa 16:00 GMT na watumiaji kuanza kupata huduma hizo karibu mwendo wa saa 22:00 GMT.

Katika taarifa Jumanne, Facebook ilisema kuwa mabadiliko mabaya ya usanidi yaliathiri zana na mifumo ya ndani ya kampuni ambayo ilikuwa vigumu kujaribu kusuluhisha shida.

Iliongeza kuwa hakuna “ushahidi kwamba data ya watumiaji imeathiriwa kutokana na wakati huu kukatika kwa huduma “.

Siku ya Jumatatu, Facebook ilituma ujumbe wa kuwaomba msamaha kwa wale walioathiriwa na kukatika kwa huduma zake .

Watu wengine pia waliripoti shida kutumia huduma nyingine zinazotegemea Facebook kama Oculus, na programu ambazo zinahitaji kuingia kwa Facebook ziliathiriwa, pamoja na Pokémon Go.

Kukatika kwa kiwango hiki kwa muda mrefu ni nadra. Usumbufu mnamo 2019 uliacha Facebook na programu zake zingine kutoweza kufikiwa kote ulimwenguni kwa zaidi ya masaa 14.

Kampuni zingine kadhaa za teknolojia, pamoja na Reddit na Twitter, zilichekelea facebook kwa shida hizo – ikisababisha majibu kutoka kwa programu zilizoathiriwa.

Usumbufu huo unakuja siku moja baada ya mahojiano na mfanyakazi wa zamani wa Facebook ambaye alivuja nyaraka kuhusu kampuni hiyo.

Frances Haugen aliliambia shirika la habari la CBS Jumapili kwamba kampuni hiyo ilikuwa imeweka kipaumbele “ukuaji juu ya usalama”.

Siku ya Jumanne atatoa ushahidi mbele ya kamati ndogo ya Seneti katika kikao kinachoitwa “Kulinda Watoto Mitandaoni”, juu ya utafiti wa kampuni hiyo juu ya athari ya Instagram kwa afya ya akili ya watumiaji wachanga.

line
Uchambuzi wa James Clayton,Ripota wa Teknolojia wa Marekani Kaskazini

Kukatika kwa huduma za mitandao mikubwa ya kijamii sio jambo geni . Wki moja iliyopita kwenye huduma za mtandao wa Slack zilikatika kwa muda.

Kinachofanya hii ijulikane sana ni kiwango na muktadha.

Hitilafu ambazo huhusisha mfumo wa jina la la domain hutatuliwa haraka. Mara nyingi pia huwekwa ndani, na watu wengine hawawezi kufungua wavuti ambayo inaweza kutazamwa katika nchi nyingine.

Ukatikaji huu, hata hivyo, ulikuwa wa ulimwengu mzima , na uliathiri kila njia nyingi za Facebook.

Urefu wa muda ambao huduma hiyo ilipotea pia sio kawaida. Kulikuwa na ripoti za “ghasia” katika makao makuu ya Facebook, wakati mafundi walipofanya kila juhudi kurekebisha shida.

Wiki ilikuwa tayari imeanza vibaya kwa Facebook- baada ya mfichuzi katika kinachoitwa “Facebook Files” kujitambulisha siku ya Jumapili.

Lakini wiki sasa imekuwa mbaya zaidi kwa mtandao huo wa kijamii.

Related Articles

Back to top button