AfyaHabari

Homa ya Nyani yaongezeka barani Ulaya

Mkuu wa shirika la afya ulimwenguni WHO kanda ya Ulaya Dr. Hans Kluge, ameonya kwamba visa vya homa ya nyani vimeongezeka mara tatu ndani ya wiki mbili zilizopita Ulaya huku Afrika ikiuchukulia ugonjwa huo kwa dharura.

Kluge amesema katika taarifa yake kuwa jitihada za makusudi zinahitajika na kuyataka mataifa kuongeza juhudi na kuhakikisha kuwa ugonjwa huo hausambai kwa kasi.  “Hatua za haraka na zilizoratibiwa ni muhimu ikiwa tunataka kukabiliana na kuenea kwa ugonjwa huu unaoendela”, alisema Kluge.

Wiki iliyopita, WHO ilisema kamati yake ya dharura ilihitimisha kuwa kuenea kwa mlipuko wa ugonjwa huo kunatia wasiwasi, lakini bado haikutoa kibali cha kutangazwa kuwa dharura ya afya duniani

Hadi kufikia sasa visa 5,000 vya homa ya nyani vimeripotiwa katika nchi 51 duniani kote kulingana na kituo cha kuzuia na kudhibiti magonjwa cha Marekani. Asilimia 90 ya visa hivyo duniani vimeripotiwa katika nchi 31 za Ulaya. Watu wengi wameripoti dalili za kupata harara, homa, uchovu, maumivu ya misuli, kutapika na baridi.

Barani afrika nako hali ikoje?

Mamlaka za afya barani Afrika zimedai kuwa zinachukulia kuenea kwa ugonjwa huo wa Homa ya Nyani kama dharura na kuyataka mataifa tajiri kushirikiana upatikanaji wa chanjo katika juhudi za kuepuka kukosekana kwa usawa kulikoshuhudiwa wakati wa janga la mlipuko wa COVID-19.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents