Siasa

Hong Kong kuchagua kiongozi mpya kuchukua nafasi ya Carrie Lam

Mkuu wa zamani wa usalama aliyesimamia oparesheni dhidi ya vuguvugu la kudai demokrasia mjini Hong Kong, John Lee anatarajiwa kuchaguliwa kuwa kiongozi mpya wa kisiwa hicho cha biashara na kamati ndogo ya wanasiasa wanaoiunga mkono China.

John Lee mwenye umri wa miaka 64, alikuwa mgombea pekee anayeungwa mkono na Beijing katika kinyanganyiro cha kumrithi kiongozi anayeondoka Carrie Lam.

Kuchaguliwa kwake, kutamuweka afisa huyo wa usalama katika wadhifa wa juu kwenye kisiwa hicho kwa mara ya kwanza kufuatia miaka kadhaa ya mvutano wa kisiasa na vizuizi vya janga la ugonjwa wa UVIKO-19.

Kiongozi wa Hong huchaguliwa na kamati maalum ya uchaguzi, inayojumuisha watu 1,463 ambao ni takriban asilimia 0.02 ya idadi jumla ya wakaazi wa jiji hilo.

Kamati hiyo, inayojumuisha wanasiasa wasomi na wafanyibiashara waliochaguliwa kutokana na utiifu wao kwa serikali mjini Beijing, watapiga kura leo Jumapili.Lee anahitaji wingi mdogo tu wa kura, lakini bila ya kuwepo mpinzani, ushindi wake unaonekana kuwa dhahiri.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents