HabariMichezo

Houngnandande pilato US Monastir Vs Yanga

Kikosi cha Young Africans kinatarajia kutupa karata yake ya kwanza kwenye Michuano ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika Jumapili ya Februari 12, 2023 dhidi ya US Monastir.

Mwamuzi, Djindo Louis Houngnandande wa Benin ndiye pilato wa mchezo huo ambao Wananchi watakuwa ugenini kwenye dimba la Stade Olympique de Radès pale Tunis.

Houngnandande ni mwamuzi ambaye dakika 90 haziwezi kukamilika bila ya kutoa kadi za njano au nyekundu pindi awapo uwanjani, hii ni kwa mujibu wa takwimu zake zinavyoonekana.

Kwa mujibu wa takwimu mwamuzi, Houngnandande ametoa kadi 51 za njano, na moja (1) nyekundu ambayo ilikuwa kwenye mechi baina ya timu ya Salitas dhidi ya Bouenguidi ambapo ilikuwa na njano 5, nyekundu 1 na mchezo kumalizika kwa goli 3-1.

Imeandikwa na @fumo255

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents