Habari

Hukumu ya Kifo yapigwa marufuku Guinea ya Ikweta

Guinea ya Ikweta imepiga marufuku hukumu ya kifo.

Televisheni ya taifa hilo imetangaza jana Jumatatu kwamba hukumu ya kifo imepigwa marufuku kabisa baada ya rais wa Guinea ya Ikweta Teodoro Obiang Nguema Mbasogo kutia saini sheria mpya.

Makamu wa rais wa nchi hiyo Teodoro Nguema Obiang Mangue ameandika kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa twita kuthibitisha hatua hiyo.

Sheria hiyo mpya itaanza kutekelezwa katika kipindi cha siku 90 baada ya kuchapishwa katika gazeti rasmi la serikali na baada ya kuridhiwa na bunge.

Kwa mujibu wa shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu Amnesty International hukumu ya kifo ilitekelezwa rasmi mara ya mwisho nchini Guinea ya Ikweta mnamo 2014.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents