Huu ndio uamuzi wa Tip Top kuhusu Dogo Janja baada ya kulalamika kuwa wanambania
Baada ya kuvuja kwa sauti ya Dogo Janja akilalamika (kwa demu) kuhusu uongozi wake wa Tip Top connection kumbania, Madee ametoa uamuzi walioamua kuuchukua.
Madee alianza kwa kusema kuwa hakuwa na taarifa yoyote juu ya malalamiko yoyote ya Dogo Janja kubaniwa mpaka alipokutana nayo kwenye audio hiyo iliyosambaa mitandaoni, na kuongeza kuwa siku moja kabla ya audio hiyo kuvuja alikuwa na Dogo Janja wakimalizia video ya wimbo wake mpya na hakujua kama kuna tatizo lolote.
Hii ndio kauli ya Madee kuhusu uamuzi wa Tip Top juu ya Janjaro;
“Mimi nabaki kwenye maamuzi ambayo tumeshaongea na Tale, kwamba hatuwezi kutoa maamuzi ambayo wao wanadhania yatakuwa ni ya kumkandamiza moja kwa moja Dogo Janja, kwa sababu sawa, mwanaume kama mwanaume unapoamua kutongoza unatumia mbinu zako nyingine nyingi tu, yeye ndio ile mbinu ambayo aliona anaweza.” alisema Madee.
“Lakini kama kazi zake sisi tumezifanya na tumeshafanya kila kitu video tayari kwahiyo sidhani kama kweli yale maneno yametoka moja kwa moja kwenye moyo wake kina Madee wananibania wakati tayari kazi zake zimeshafanywa na ratiba yake imeshafanywa, nachoamini mimi ni kwamba alikuwa anataka kumuwin tu Yule mwanamke, lakini kikubwa ambacho amehaaribui ni matusi pamoja na kutoa siri ambazo yeye anaona ni sawa kuzisema.” Alieleza Madee.
Licha ya Janjaro kufanya hayo, Madee amesema kuwa hawatasitisha kutoa kazi zake ambazo tayari zilikuwa kwenye ratiba ya kutoka.
“ratiba lazima ziendelee kwasababu tayari tumeshapata hasara tumeshatoa hela za kufanya audio , video ratiba itaendelea lakini lazima Dogo Janja atakuwa chini ya adhabu.” alisema Mdee
Msikilize zaidi Madee kwenye mahojiano na Millard Ayo.